SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la umoja wa Mataifa-UNESCO– kwa kushirikiana na wizara ya habari, vijana, utamaduni na michezo nchini wameungana kuongoza sherehe za wiki ya kumbukumbu ya wiki ya ukombozi wa bara la Afrika zinazoanza leo hadi mei 29 mwaka huu maeneo mbalimbali ya Afrika.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika hilo sherehe hiyo hufanyika kila ifikapo mei 25 ya kila mwaka ndani na nje ya bara la Afrika kukumbuka siku ambayo viongozi wa bara hilo walipokutana mwaka 1963 na kuanzisha jumuiya ya umoja wa nchi huru za Afrika.
Sherehe hizo zinalenga zaidi shughuli mbalimbali zitakazoleta chachu ya kuongeza kiwango kwa mwananchi kutambua umuhimu wa siku hiyo ikiwa ni sehemu ya urithi wa Afrika.