WATANZANIA wameombwa kutunza miradi mbalimbali ya mandeleo inayoletwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau na wananchi wenyewe.
Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Juma Chumu alipokuwa akizindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Ilala yenye gharama ya shilingi bilioni 14.
Aidha amewataka watanzania kuepuka kutumiwa na wanasiasa ili kusababisha uvunjifu wa amani katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.