SERIKALI ya China imepiga marufuku uvutaji wa sigara katika maeneo yote ya wazi katika mji wa Beijing.
Maelfu ya maafisa wameanza kufanya ukaguzi katika maeneo yote yaliyoanishwa kutohusika na kitendo cha uvutaji sigara ambapo kwa wale watakaokiuka kufuata sheria hiyo watapigwa faini.
Hata hivyo tafiti zinasema kuwa China ina jumla ya wavutaji sigara milioni 300 wakati sheria ya kusitisha uvutaji sigara katika maeneo ya wazi ya mji wa Beijing ilipopitishwa kwa mara ya kwanza na kushindwa kutekelezeka.