RAIS mstaafu wa Burundi DOMITIEN NDAYIZEYE amemtaka rais wa sasa wa nchi hiyo PIERRE NKURUNZINZA kutogombea kwa muhula wa tatu kwani hatua hiyo inavunja maridhiano yaliyofanyika yaliyomtaka rais huyo kukaa madarakani kwa mihula miwli.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam katika mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika mashariki amesema kuwa mkataba uliosainiwa umebainisha kila makubaliano waliyoafikiana lakini hatua inayofanywa sasa na rais NKURUNZINZA umesababisha ukiukwaji wa haki za binadamu.
Aidha rais huyo mstaafu amesema kuwa vurugu zinazoendelea nchini humo zimesababisha madhara makubwa kwa wananchi ikiwemo vifo, uharibifu wa mali pamoja na kufungwa kwa shule mbalimbali.