WAZIRI mkuu wa Iraq HAIDER AL-ABADI amesema kuna ushahidi mdogo wa kuwepo kwa uungwaji mkono wa kimataifa katika vita vyao dhidi ya wapiganaji wa Islamic State katika nchi yake.
Matamshi hayo ya ABADI yanakuja wakati wa kikao kinachotarajiwa kufanyika huko Ufaransa cha mataifa walioungana kulipiga vita kundi hilo la wapiganaji la Islamic state.
Aidha Waziri HAIDER AL-ABADI ameonya kuwa kinyume na matarajio wanamgambo hao wa kundi la IS wanaendelea kuwasajili watu wengi ili kujiunga nao.