FRENCH OPEN KUWAKUTANISHA WAKALI WA TENIS DUNIANI

FRENCH OPEN KUWAKUTANISHA WAKALI WA TENIS DUNIANI

Like
277
0
Wednesday, 03 June 2015
Slider

Rafael Nadal bingwa mara tisa wa michuano hiyo anavaana na Djokovic mchezaji nambari moja kwa ubora. Nadal Mhispania amewahi kumshinda Mserbia Djokovic mara sita katika michuano hiyo siku za nyuma.

Huu unaelezwa kuwa mpambano mkali zaidi katika michuano ya French Open inayoendelea katika viwanja vya tenis mjini Paris ukiwemo uwanja wa Roland Garros.

Mchezaji nambari mbili kwa ubora katika mchezo huo duniani kwa wanaume na bingwa wa mwaka 2009 Roger Federer ameng’olewa katika michunao hiyo hatua ya robo fainali baada ya kucharazwa na Stan Wawrinka kwa seti 6-4 6-3 7-6 (7-4).

Wawrinka, mwenye umri wa miaka 30, amewahi kupoteza michezo yote minne walipokutana na Federer katika michuano hiyo mikubwa.

Lakini Wawrink ambaye ni wa nane kwa ubora katika tenis amemwangusha Federer mwenye umri wa miaka 33 ambaye alikuwa mchezaji mwenza katika michuano ya Kombe la Davis.

Kwa matokeo hayo Wawrinka atapambana hatua ya nusu fainali na Mfaransa Jo-Wilfried Tsonga ambaye anapewa nafasi kubwa kufuatia ushindi wake dhidi ya Mjapan Kei Nishikori.

Tsonga alipata kibarua kigumu kumng’oa mpinzani wake Nishikori alipopata matokeo ya kufunga seti tatu dhidi ya mbili yaani 6-1 6-4 4-6 3-6 6-3.

Kwa upande mwingine Andy Murray leo atajaribu kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya French Open kwa mara ya tatu katika siku ambayo Novak Djokovic na Rafael Nadal wanapambana mjini Paris.

Murray wa tatu kwa ubora duniani anacheza dhidi ya Mhispania David Ferrer anayeshika nafasi ya saba kwa ubora.

Murray amesema hilo litakuwa pambano kali na mtihani mkubwa kwake.

Comments are closed.