KATIKA kuelekea wiki ya Utumishi wa Umma nchini Wakala wa usajili na udhibiti wa Vizazi na Vifo- RITA-imewataka wananchi kuwa na tabia ya kuandika wosia katika familia zao ili kuepusha utata na migogoro ya mara kwa mara inayoweza kujitokeza mara baada ya mtu kufariki.
Akizungumza na efm Meneja Masoko, Mawasiliano na Elimu kwa Umma kutoka –Rita– JOSEPHAT KIMARO amesema kuwa kumekuwa na dhana kwa jamii kuwa mtu akiandika wosia anajitabiria kifo jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo katika familia nyingi.
Aidha amebainisha kuwa mtu anaweza kuandika wosia na kuishi kama alivyopanhiwa kwani kuandika wosia kunamuwezesha mlengwa kumchagua msimamizi wa mirathi mapema ikiwa ni pamoja na kutoa uhakika wa familia kunufaika na mali na kuepusha migongano katika jamii.
*****
WANAMGAMBO wa kiislamu nchini Nigeria wametoa picha mpya za video lakini Kiongozi wa Boko Haram ambaye huwa anaonekana kwenye video zao, ABUBAKAR SHEKAU hakuonekana kwenye picha hizo.
Imeelezwa kuwa kutoonekana kwa Shekau kwenye Video hiyo kumeleta hali ya wasiwasi kuhusu kuwepo kwa mgawanyiko ndani ya kundi hilo.
Hata hivyo katika picha ya video ya dakika 10imeonesha msemaji huyo anakanusha taarifa zilizotolewa na Jeshi la Serikali kuwa linadhibiti miji yote kutoka mikononi mwa wanamgambo.