WAZIRI wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu amesema kuwa matumizi mabaya ya ardhi yasiyozingatia mpango bora yamekuwa tishio kwa maeneo yanayozunguka hifadhi za jamii.
Nyalandu ameyasema hayo wakati akihutubia mkutano kati ya Wizara na Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori –WMAs– uliofanyika jijini Arusha ambapo amesema kuwa ili kuwa na uhifadhi endelevu utakaorithiwa na vizazi vijavyo mpango wa matumizi bora ya ardhi hauna budi kuzingatiwa.
Aidha amesema kuwa ujenzi wa miji katika maeneo ya hifadhi ikiwemo Hoteli na kumbi za starehe unaathiri shughuli za uhifadhi na kuwataka wadau wa utalii kugawanya uwekekezaji kwa kuwekeza nje ya hifadhi.