WATU 29 wamefariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipundupindu nchini Sudan Kusini huku wengine elfu moja wakiwa katika hatari ya kuambukizwa ugonjwa huo.
Takriban visa 484 vya ugonjwa huo ikiwemo vifo 29 ambavyo sita kati yake ni vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano idadi iliyoripotiwa mwishoni mwa mwezi Juni kutoka ofisi ya mratibu wa masuala ya kibinaadamu katika umoja wa kimataifa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo watoto elfu tano walio chini ya umri wa miaka mitano wako hatarini kupoteza maisha kutokana na ugonjwa huo ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa za kupambana nao.