HATIMAYE Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imewahukumi kifungo cha Miaka mitatu jela Mawaziri waandamizi wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona.
Hata hivyo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Hazina, Gray Mgonja ameachiwa huru baada ya Mahakama kumwona hana hatia.
Viongozi hao walikuwa wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7.