WATANZANIA WAMETAKIWA KUTOFANYA MAKOSA KATIKA UCHAGUZI MKUU

WATANZANIA WAMETAKIWA KUTOFANYA MAKOSA KATIKA UCHAGUZI MKUU

Like
208
0
Tuesday, 07 July 2015
Local News

WATANZANIA wametakiwa kutofanya makosa katika uchaguzi mkuu ujao kwa kuchagua wabunge watakaoweza kuhimili changamoto na kujenga hoja katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Rai hiyo imetolewa leo na Naibu katibu Mkuu wa Chama cha-Alliance For Democratic ChangeADC– Doyyo Hassan Doyyo wakati akizungumza na EFM juu ya sakata la wabunge wa Upinzani kutoka nje ya Bunge kwa kupinga miswada  iliyowasilishwa bungeni kwa hati ya dharula.

Aidha amesema kuwa kutokana na umuhimu wa miswada hiyo ambayo inawagusa watanzania wote wabunge walipaswa kupinga kwa hoja na si kutoka nje kama walivyofanya kwani kwa kufanya hivyo wameonesha udhaifu wa kiuongozi.

Comments are closed.