IMEELEZWA kuwa zaidi ya ajira elf 16 zinatarajiwa kuzalishwa kutokana na kuanzishwa kwa shughuli za ujenzi wa mitambo ya mafuta na gesi nchini Tanzania.
Akizungumza na kituo hiki Jijini Dar es salaam Mkufunzi wa umeme kutoka chuo cha –VETA– mkoani Lindi MAJEO MGOE amesema shughuli hizo zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza Ajira hususani kwa wahitimu wa chuo hicho.
Magoe ameongeza kuwa mafunzo wanayopata wanafunzi kutoka katika chuo hicho yamewasaidia vijana kuongeza sifa za kuajiriwa hali ambayo inawawakwamua kiuchumi na kuliletea Taifa maendeleo.