SERIKALI ya Ugiriki ipo katika harakati za kuandika mapendekezo mapya yatakayofanikisha mazungumzo ya kutafutia ufumbuzi wa matatizo yake ya kiuchumi.
Hali hiyo imekuja kufuatia viongozi wa Ukanda wa Ulaya mjini Brussels kuipa nchi hiyo muda wa siku tano kupeleka mapendekezo yake ya kusaidia kuondokana na tatizo la uchumi.
Mbali na nchi hiyo kupewa muda huo wa kupeleka mapendekezo yake lakini Raisi wa baraza la viongozi wa ukanda wa ulaya Donuld Tusk ameonya kuwa zimesalia siku chache kutatua mgogoro wa Ugiriki na endapo isipowezekana utaratibu wote utaharibika.