SERIKALI imeridhia kuanzishwa kwa baadhi ya wilaya na mikoa mipya kwa lengo la kusogeza karibu huduma muhimu kwa wananchi ili kuleta manufaa kwa Taifa.
Akizungumza wakati akitoa hoja ya kuahirisha kikao cha bunge Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Mizengo Pinda amezitaja baadhi ya wilaya mpya kuwa ni Ubungo na Kigamboni za Jijini Dar es salaam.
Waziri Pinda amesema kwamba mpango huo wa kuongeza wilaya na mikoa mipya utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha utendaji wa shughuli za serikali.