MAZUNGUMZO kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yemeendelea hadi usiku wa kuamkia leo mjini Vienna kujaribu kufikia makubaliano yatakayoweza kuudhibiti mpango huo na kuizuia Iran kutengeneza silaha za atomiki.
Msemaji wa ikulu ya Marekaani Josh Earnest amesema kuwa baadhi ya masuala muhimu yameshughulikiwa, lakini bado kuna masuala mengine yanayoendelea kuleta mzozo.
Ikiwa kuna muafaka kuhusu vipengele vyote vya makubaliano hayo, wanadiplomasia wakuu kutoka baadhi ya mataifa makubwa ikiwemo Iran, Marekani, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani watakusanyika mjini Vienna kwa ajili ya mkutano wa mwisho.