WAUMINI wa Dini ya Kiislamu pamoja na Watanzania kwa ujumla wametakiwa kuzidisha mshikamano na umoja hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea kwenye uchaguzi mkuu.
Hayo yamesemwa Jijini Dar es salaam na Sheikh Mkuu wa Mkoa huo ALHAD MUSSA SALIM alipo kuwa anatoa mwaliko wa kuswali pamoja swala ya idd el fitr kwa waumini wa dini hiyo katika viwanya vya mnazi mmoja ambayo itategemea na kuandama kwa mwezi kati ya tarehe 17 au 18.
Alhad amesema kuwa sikukuu hiyo ni siku ya kutoa zakatul fitr kabla ya swala ya idd kuswaliwa kwa kuwakumbuka mayatima , wajane , mafakiri na maskini na kuwapa misaada mbalimbali.