TARIME: MADIWANI WAITAKA HALMASHAURI KUJENGA SHULE ZA KUTOSHA KWA AJILI YA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM

TARIME: MADIWANI WAITAKA HALMASHAURI KUJENGA SHULE ZA KUTOSHA KWA AJILI YA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM

Like
195
0
Thursday, 16 July 2015
Local News

KATIKA kutambua umuhimu wa watu wenye mahitaji maalumu wakiwemo  walemavu wa vioungo mbalimbali , Madiwani wa Halmshauri ya Mji wa Tarime Mkoani  Mara wameitaka Halmshauri hiyo kujenga shule za kutosha  kwa ajili ya walemavu hao.

Hata hivyo wameitaka pia jamii nzima kuondokana na utamaduni wakudhani kuwa ulemavu ni mkosi katika familia na kutowaficha watu hao na badala yake wawapeleke shule kwa lengo la kupata Elimu kwani ni haki yao ya Msingi.

Kauli hiyo ya Madiwani imetolewa katika kikao chao cha kuvunja Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa NTC Wilayani humo.

Comments are closed.