MBIO ZA UBUNGE CCM ZAANZA DAR

MBIO ZA UBUNGE CCM ZAANZA DAR

Like
207
0
Friday, 17 July 2015
Local News

JUMLA ya wanachama 36 wa chama cha mapinduzi-CCM-wamejitokeza kutaka kugombea nafasi za ubunge kupitia chama hicho katika majimbo manne ya Kinondoni, Kawe, Ubungo na Kibamba.

 

Hayo yamesemwa na katibu wa –CCM– wilaya ya kinondoni ATHUMAN SHESHA alipokuwa akizungumza na kituo hiki ambapo amesema kuwa hadi sasa jimbo la Kawe linaongoza kwa kuwa na wagombea wengi wapato 15.

 

SHESHA amesema kuwa kila mgombea aliyefika kuchukua fomu amepewa mashariti ya kugombea nafasi hiyo ikiwa ni pamoja na kujiepusha na vitendo vya utoaji rushwa kwa wajumbe na kutofanya kampeni kabla ya muda muafaka.

Comments are closed.