KUSHIRIKISHA WANANCHI KIKAMILIFU KWENYE NGAZI ZA MAAMUZI NI CHACHU YA MAENDELEO

KUSHIRIKISHA WANANCHI KIKAMILIFU KWENYE NGAZI ZA MAAMUZI NI CHACHU YA MAENDELEO

Like
175
0
Monday, 20 July 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa ili kuleta maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii katika majimbo mbalimbali yanayoongozwa na viongozi wa siasa nchini hususani wabunge, Viongozi hao wanapaswa kufuatilia kwa umakini shughuli zote za kiutendaji zinazofanyika kwenye majimbo yao pamoja na kuwashirikisha wananchi kikamilifu kwenye ngazi za maamuzi.

Hayo yamesemwa Jijini Dar es Salaam na Mwanachama wa Chama cha Mapinduzi-CCM, CHRISTOPHER JAFET alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya nia yake ya kugombea nafasi ya ubunge wa Jimbo la Segerea kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi-CCM.

Amebainisha kuwa endapo chama kitampa ridhaa ya kumpitisha kuwa mgombea wa jimbo hilo akiwa kama kiongozi atahakikisha anarekebisha mapungufu yote yaliyojitokeza jimboni hapo kwa kipindi chote cha uongozi uliopo ikiwa ni pamoja na kurekebisha miundombinu ya barabara, maji, umeme, elimu na Afya kwani imekuwa changamoto kubwa jimboni humo.

Comments are closed.