JUMLA ya watu 39 kutoka nchini Afrika Kusini wameshiriki katika zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro lenye lego la kuchangisha fedha za kusaidia Afya ya watoto wa kike huku sehemu kubwa ya fedha hizo zimelenga kusaidia watoto wa kike laki 2 na elfu 72 wa Afrika Kusini pamoja na Tanzania wanaoishi katika vijiji vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa ya Mlima huo.
Ugeni huo uliopanda Mlima Kilimanjaro Julai 14 mwaka huu umejumuisha watu mbalimbali wakiwemo wakurugenzi wa kampuni ya Vodacom na waigizaji maarufu wa Filamu wa nchini Afrika kusini.
Mkurugenzi wa Utalii wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania –TANAPA- Ibrahim Musa amesema tayari amefanya mazungumzo na muigizaji maarufu kutoka nchini Afrika kusini Rajesh Kumar namna ambavyo atakavyo saidia kutangaza vivutio vya utalii ili kuleta manufaa kwa Taifa.