ASILIMIA 70 YA WAGONJWA WA SARATANI HUPOTEZA MAISHA KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA

ASILIMIA 70 YA WAGONJWA WA SARATANI HUPOTEZA MAISHA KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA

Like
233
0
Tuesday, 21 July 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa asillimia 70 ya wagonjwa wa saratani hupoteza maisha katika nchi zinazoendelea na katika Bara la Afrika lenye watu zaidi ya milioni 804 asilimia  12.4 wanapata saratani kabla ya kufikia umri wa miaka 75  na asilimia  90 wanapata ugonjwa huo wakiwa na  umri chini ya miaka 40.

 

Hayo yamesemwa na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati akifungua mkutano wa tisa wa Jukwaa la wake wa marais wa Afrika la kutokomeza magonjwa ya saratani za mfumo wa uzazi ambazo ni mlango wa kizazi, matiti na tezi dume unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa-KICC– mjini Nairobi.

 

Rais Kenyatta amesema Ripoti ya saratani iliyotolewa mwaka 2014 na  Shirika la Kimataifa la kutafiti ugonjwa huo kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani –WHO– ilionesha kuwa takwimu mpya za saratani zinaongezeka  kila mwaka na kwa upande wa Afrika  vifo vingi vinatokana na saratani ya mlango wa kizazi.

S1 S2

Comments are closed.