SERIKALI ya Ugiriki imefanikiwa kuwasilisha sehemu ya malipo ya deni lake kwa Shirika la Fedha la Kimataifa –IMF– hali inayoashiria kutokuwepo tena kwenye hatari ya kufilisika.
Msemaji wa –IMF– Gerry Rice amesema katika taarifa yake muda mfupi uliopita kwamba Ugiriki imelipa euro bilioni 2 jana ambapo Kamisheni ya Ulaya iliruhusu nchi hiyo kupatiwa mkopo wa euro bilioni 7 ili kuiwezesha serikali ya waziri Mkuu Alexis Tsipras kulipa sehemu ya madeni yake kwa Benki Kuu ya Ulaya na IMF.
Msemaji wa Kamisheni ya Ulaya Mina Andreeva aliwaambia waandishi wa habari mjini Brussels kwamba sasa ni haki kwa Ugiriki kuchukua hatua muafaka kupata fedha hizo,