ALIEKUA Diwani wa Kata ya Kunduchi kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA- ambae pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama hicho -BAWACHA-jimbo la Kawe Janeth Rithe ameachana na chama hicho na kujiunga na chama cha ACT WAZALENDO akiambatana na Viongozi wenzake 12 wa jimbo la Kawe.
Akiongea na Waandishi wa Habari Mara baada ya kukabidhiwa kadi ya Chama cha ACT WAZALENDO Rithe amesema amechukua uamuzi huo baada ya kusoma sera na kugundua kua hicho ndio chama kinachosimamia demokrasia ya kweli tofauti na vyama vingine vya siasa.
Kwa upande wake Naibu katibu Mkuu wa ACT WAZALENDO Msafiri Mtemelwa amesema kila Mtanzania ana haki ya kuhamia ama kujiunga na chama chochote anachokitaka kwani vyama hivyo sio dini.