KAMISHINA wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa amesisitiza haja ya kuhakikisha kwamba viwango vya umahiri vya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini vinakua vya juu kukidhi haja ya matumizi ya kufundishia na kujifunza nchini.
Ametoa kauli hiyo mjini Bagamoyo wakati akifungua kongamano linalohusu upitiaji waraka wa mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu.
Katika hotuba yake iliyosomwa na Kaimu Kamishina wa Elimu, Benjamin Kulwa amesema kwamba changamoto ya Tehama inaonekana wazi katika matumizi yake na hivyo wakufunzi lazima wawe mahiri.