WIZARA YA NISHATI NA MADINI IMEANDAA MUFUNZO KUEPUSHA MIGONGANO KANDA YA KASKAZINI

WIZARA YA NISHATI NA MADINI IMEANDAA MUFUNZO KUEPUSHA MIGONGANO KANDA YA KASKAZINI

Like
265
0
Tuesday, 28 July 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa ili kuondokana na migongano kwenye usimamizi wa sekta ya madini Kanda ya Kaskazini, Wizara ya Nishati na Madini imeandaa mafunzo kuhusu sekta ya madini yatakayoshirikisha viongozi mbalimbali katika mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro yatakayofanyika Agosti 12 mwaka huu.


Akizungumza katika mahojiano maalum jijini Arusha Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Kilimanjaro Fatuma Kyando amesema kuwa mafunzo hayo yatashirikisha wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, maafisa tawala wa wilaya, watendaji na wawakilishi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania –TRA.


Aidha ameeleza kuwa katika usimamizi wa sekta ya madini wa kanda hiyo, kumekuwepo na mgongano wa mamlaka ambapo kila upande umekuwa ukiona una nguvu kuliko mwingine katika utoaji na usimamizi wa leseni za madini.

Comments are closed.