TIMU YA SPECIAL OLYMPICS TANZANIA YANG’AA MAREKANI

TIMU YA SPECIAL OLYMPICS TANZANIA YANG’AA MAREKANI

Like
447
0
Friday, 31 July 2015
Slider

Timu ya Taifa (Special Olympics Tanzania) iliyoko Los Anegels – Marekani imeendelea kupata mafanikio makubwa baaba ya siku ya jana tarehe 30 Julai kujipatia jumla ya medali tano.

 

Medali hizo zimepatikana kupitia michezo na wachezaji wafuatao:

 

  1. Blandina Patrick m. 800 (wk) – Alipata medali ya Dhahabu
  2. Deonatus Manyama m. 800 (wm)- Alipata medali ya Fedha
  3. Riziki Chilumba m. 100 (wk) – Alipata medali ya Fedha
  4. Aisha Kaoneka m. 100 (wk) – Alipata medali ya Shaba
  5. Faraja Meza M. 100 (wk) – alipata medali ya Dhahabu

 

Kwa ushindi huu, ukijumlisha na ushindi wa juzi wa medali tatu, Tanzania imefikisha jumla ya medali 8 zikiwemo:

 

– Dhahabu  – 3

– Fedha      – 3

– Shaba      – 2

 

Leo tarehe 31 Julai, Watanzania wengine watakuwa uwanjani kusaka medali zaidi. Hawa ni:

 

  1. Bonaventura Anga – m. 5,000 (wm)
  2. Godfrey Jabuya m 100 (wm)
  3. David Kenyamaho m. 100 (wm)
  4. Aisha Kaomeka m. 200 (wk)
  5. Faraja Meza m. 200 (wk)

 

Pichani ni baadha ya washindi.

 

Frank Macha,

MKUU WA MSAFARA,

TIMU YA TAIFA – SPECIAL OLYMPICS,

LOS ANGELES – USA.

 

 

Timu hiyo yenye jumla ya wachezaji nane ambao wanashiriki kwenye mchezo wa riadha katika mita 100, 200, 4000 na 5000 katika mashindano ya dunia

IMG_5119[1]

IMG_5117[1]

 

Comments are closed.