CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema nafasi yoyote ya kukiondoa Chama cha Mapinduzi CCM madarakani ni lazima itumike kwa kutambua kuwa Chadema ni chama cha watu, na hivyo ni lazima waheshimu mawazo ya kila mtu mwenye lengo linalofanana na chama hicho.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam katika Mkutano wa baraza kuu la Chama cha Maendeleo na Demokrasia CHADEMA uliofanyika ili kupitia na kuijadili ilani ya uchaguzi ambayo itapendekezwa katika mkutano mkuu kesho tarehe 4 Agosti 2015.
Akizungumza katika Mkutanohuo Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Freeman Mboye amesema ilikuwa lazima kama chama cha siasa kuweka mkakati wa kila wanayeweza kumpokea kutoka chama kingine ambacho sio mshirika wa UKAWA achukuliwe ili waweze kuunganisha Watanzania wote wenye mawazo chanya na nia ya dhati kwa Taifa.