CHAMA CHA MADEREVA KIMETISHIA KUFANYA MAAMUZI MAZITO AGOSTI 9

CHAMA CHA MADEREVA KIMETISHIA KUFANYA MAAMUZI MAZITO AGOSTI 9

Like
172
0
Tuesday, 04 August 2015
Local News

CHAMA cha Wafanyakazi madereva Tanzania-TADWU kimesema endapo vipengele viwili vya maboresho ya mishahara na posho havitazingatiwa kulingana na makubaliano walioafikiana katika kikao cha juni 21 mwaka huu baina ya kamati ya kudumu, Sumatra na Wamiliki wa vyombo vya usafiri chama hicho kitatoa maamuzi mazito ifikapo tarehe 9 Agosti mwaka huu.

Akizungumza na Efm jijini Dar es salaam Katibu na Msemaji wa TADWU Rashid Salehe amesema kikao cha mwisho kilikubaliana kuwa ifikapo tarehe 1 Julai mikataba mipya iliyoundwa kwa pamoja ianze kutumika jambo ambalo limeenda kinyume na makubalino.

Aidha Katibu Salehe amebainisha kuwa wamiliki wa vyombo vya moto nchini ni viongozi wa juu wa nchi hii hivyo ni vigumu sana bila kutumia umoja wao wa madereva wa TADWU kuweza kupata haki zao za msingi.

Comments are closed.