Charlie Austin, mshambuliaji wa Queens Park Rangers aliyeitwa kuchezea timu ya taifa ya Uingereza mwishoni mwa msimu uliopita, huenda akahama klabu hiyo iliyoshushwa daraja kabla ya mwisho wa kipindi cha kuhama wachezaji, meneja wa klabu hiyo Chris Ramsey alisema Jumatatu.
Kiungo wa kati Leroy Fer pia sana huenda akahama, ingawa Ramsey anatumai wawili hao wanaweza bado kuwa kwenye klabu hiyo na kucheza mechi yao ya kwanza ya Championship (ligi ya daraja la pili) ugenini London dhidi ya Charlton Jumamosi.
“Tunajua ni tatizo la kifedha kwa wachezaji hao, wakipewa ofa nzuri, sanasana huenda wakaondoka,” aliambia kituo cha redio cha BBC London 94.9.
“Lakini moyoni, naomba kusiwe na mtu wa kuja kuwatafuta. Yeyote aliye nasi hapa na anaweza kusaidia tunamhitaji. Kinachofanyika ni kwamba wachezaji wanafanya mazoezi makali sana kujiweka sawa kwa ajili ya mwanzo wa msimu na iwapo watakuwa sawa basi watacheza.”
Austin alikuwa ndiye mfungaji mabao bora wa QPR msimu uliopita akiwafungia mabao 18 ingawa walimaliza msimu wakishika mkia Ligi ya Premia.
Fer, kiungo wa kati wa Uholanzi, alifunga mabao sita tangu ajiunge nao kutoka Norwich City mwaka mmoja uliopita.