VIKOSI vya Usalama nchini Sudani Kusini vimefunga kituo cha redio iliyokuwa ikiunga mkono mpango wa kumaliza mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yanayoendelea nchini humo.
Mamlaka ya nchi hiyo, imekilazimisha kituo cha radio cha Free Voice South Sudan kinachoungwa mkono na Marekani kutorusha matangazo yake siku ya jana, siku moja tu baada ya kulifungia gazeti la The Citizen.
Wapatanishi wa kimataifa wamewapa rais Salva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar mpaka katikati ya mwezi Agosti kusaini makubaliano ya amani.