MAKOSA YA PETR CECH YAIGHARIMU ARSENAL

MAKOSA YA PETR CECH YAIGHARIMU ARSENAL

Like
273
0
Monday, 10 August 2015
Slider

Klabu ya soka ya Arsenal imekuwa na hali ngumu katika mchezo wa ufunguzi wa ligi ya England kufuatia makosa ya mlinda mlango Petr Cech kuiwezesha klabu ya West Ham kuweka rekodi ya kuitandika Arsenal 2-0 katika uwanja wao wa nyumbani wa Emirates

Cech alisajiliwa kutoka Chelsea huku usajili wake ukitarajiwa kuisaidia Arsenal kutwaa taji la ligi hiyo lakini kwa mchezo huo wa siku ya jumapili umefungua vibaya ujio wake kwenye klabu hiyo kufuatia rekodi yao ya kufungua michuano hiyo huku wakipokea kichapo kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka mitatu

Akizungumza baada ya mchezo huo mwalimu wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ambae klabu yake ilifanikiwa kuwatandika Chelsea mabingwa wa ligi hiyo 1-0 katika mchezo wa ngao ya hisani.

Wenger amesema huenda wachezaji waliaathiriwa na hofu na kuwa na kutawaliwa na presha ya mchezo lakini pia Wenger ameeleza kuwa wameumizwa na matokeo hayo lakini pia ni nafasi nzuri kwa wao kujipanga

Comments are closed.