WATANZANIA wameombwa kujitokeza kwa wingi katika kuchangia mfuko wa uwezeshaji watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali kwa lengo la kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili watu hao.
Akizungumza na kituo hiki Jijini Dar es salaam makamu mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu wilaya ya Temeke Shany Zubery amesema kuwa endapo suala la uchangishaji litafanikiwa litasaidia kwa kiasi kikubwa kuwasaidia watu hao.
Aidha amesema kuwa shirikisho hilo limekuwa likikabiliwa na changamoto nyingi ambazo husababisha kushindwa kuonesha mafanikio makubwa hivyo amewasisitiza watu kuchangia kupitia namba husika ili kufungua mfuko huo.