BAADA ya kumalizika kwa Tamasha la muziki mnene Bar kwa bar awamu ya kwanza, na mashabiki kuomba Burudani hiyo iendelea tena, Uongozi Efm umekubali ombi hilo na sasa Tamasha hilo linarudi tena kwa kishindo likiwa limeboreshwa kwakuongeza wigo wa kuwafikia watu wengi zaidi.
Muziki mnene bar kwa bar awamu hii bila kuwasahamu wasikilizaji na mashabiki wa EFM katika wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala kwa umuhimu wake na Wilaya mpya katika mkoa wa Dar es salaam, Muziki mnene sasa utapelekwa pia katika mkoa wa Pwani.
Maeneo ambayo wanatakiwa kukaa tayari kwa Muziki mnene bar kwa bar utakaoporomoshwa na Madjs wakali wa Efm, ni pamoja na Kibaha, Mlandizi, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe, Kigamboni na maeneo mengine mengi kwa ajili ya kuhakikisha tunakonga nyoyo za mashabiki wetu.
Muziki Mnene bar kwa bar mwaka huu inatarajiwa kuanza rasmi tarehe 5/09/2015 . Lakini katika kuelekea huko efm imeanza na Muziki mnene bango katika sehemu yako ya biashara ambako bwana E anapita na ukiwa umeweka bango la EFM na unasikiliza matangazo yetu basi utapata kifurushi chenye zawadi kibao.
Na kama ilivyokawaida yetu, mwishoni tutakuwa na Tamasha kubwa la hitimisho ambalo litafanyika jijini Dar es salaam ambalo safari hii limeboreshwa na kuongezwa vionjo vingi sana.
Denis Ssebo mkurugenzi mkuu wa mawasiliano Efm
“Ninawaomba wasikilizaji wetu wakae mkao wa kula maana tutawafikia na kuwamiminia Burudani ambayo pia itarushwa live kutoka eneo husika kupitia kituo chao cha 93.7 EFM. Njoo tuonane, tufahamiane na tuijenge Radio yetu efm ambayo kwetu Muziki unaongea”.
LAKINI jambo la pili ambalo ndugu zangu wanahabari tungependa kuwajulisha ni kwamba katika kuhakikisha tunaendelea kukupa kilicho bora zaidi kupitia vipindi vyetu mbalimbali,sanjari na kuwa na watangazaji wenye ushawishi na uwezo mkubwa. leo hii tunamtambulisha kwenu mtangazaji Dina Marios ambaye wengi uwezo wake mnaujua na sasa ameungana na wenzake wenye uwezo mkubwa katika familia ya Efm.
Picha kutoka kushoto ni Dina Marios akizungumza na waandishi wa habari
IMETOLEWA NA
DENIS SSEBO
MKURUGENZI MKUU WA MAWASILIANO – EFM.