UN YAPELEKA MAAFISA WAKE BURUNDI

UN YAPELEKA MAAFISA WAKE BURUNDI

Like
163
0
Tuesday, 11 August 2015
Global News

BARAZA la usalama la umoja wa mataifa limeunga mkono mpango wa kutuma maafisa wake wa ngazi ya juu nchini Burundi kwa ajili ya kutatua hali ya sintofahamu iliyopo nchini humo.

Baraza lililopo kwa sasa chini ya Mnigeria Joy Ogwu limesema kuwa kumekuwepo na wasiwasi mkubwa juu ya hali ya usalama nchini Burundi huku likitoa wito kwa serikali kufanya mazungumzo ya amani na upande wa upinzani.

Kiongozi mwandamizi wa umoja wa mataifa kuhusiana na haki za binaadam Ivan Simonovic ambaye alipelekwa na baraza hilo amesema hali ya uchunguzi ilikuwa ya kuzorota nchini Burundi lakini bado hawajakata tamaa.

Comments are closed.