KUTOKANA na umuhimu na wingi wa Matumizi ya Mafuta kwenye Magari na Mitambo ya serikali katika utekelezaji wa majukumu yake pamoja na gharama kubwa wakala wa huduma ya ununuzi serikalini GPSA umeamua kusimamia mfumo wa udhibiti wa mafuta katika visima na magari ya serikali.
Akizungumza na kituo hiki Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa huduma hiyo NAFTAL SINGWEJO amesema kuwa lengo kubwa la mfumo huo ni kuhakikisha kunakuwa na usimamizi bora wa matumizi ya mafuta ambao utapunguza gharama za ununuzi na matumizi ya magari hayo.