JAMII imetakiwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali zinazotoa huduma kwa watoto yatima na wanao ishi katika mazingira magumu kwani kwa kufanya hivyo itaweza kupunguza ongezeko la idadi kubwa ya watoto wa mitaani.
Akizungumza na EFM Mkurugenzi wa kituo kinacholea watoto wanaoishi katika mazingira magumu –BABA WATOTO CENTER– MGUNGA MNYENYELWA amesema kuwa mpaka sasa wameweza kulea watoto 200 kituoni hapo pamoja na kuwapatia mafunzo mbalimbali yanayohusu stadi za maisha.
Amebainisha kuwa Miongoni mwa mafunzo wanayopewa kituo ni kutoa nafasi kwa watoto wa kike kujifunza ufundi cherehani ingawa harakati hizo zimekumbana na changamoto ya upungufu wa fedha za kununulia vifaa vya mafunzo.