BOMU kubwa lililokuwa katika gari limeripuka katika soko lililokuwa na watu wengi mjini Baghdad leo na kusababisha watu 50 kuuwawa na wengine 150 wamejeruhiwa.
Polisi mjini Baghdad imesema gari hilo liliripuriwa katika soko la chakula la Jamila katika mji wa Sadr, ambao wakazi wake wengi ni Washia , Mashariki mwa Baghdad.
Maafisa wa hospitali wamesema wengi wa wahanga wamepata majeraha makubwa .