VIJANA WATAJWA KUWA CHACHU YA MAENDELEO KWA TAIFA

VIJANA WATAJWA KUWA CHACHU YA MAENDELEO KWA TAIFA

Like
171
0
Monday, 17 August 2015
Local News

IMEELEZWA kuwa Taifa linaweza kuwa na mfumo mzuri zaidi endapo litahakikisha kuwa Vijana wanauwezo wa kuajiriwa, kujiajiri au kuwa na ufundi wa kufanya mambo yao wenyewe na sio wawe wanasoma tu na kupata vyeti ambavyo wanashindwa kufanya navyo kitu chochote.

 

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue wakati wa ufunguzi wa warsha ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyoshirikisha wadau mbalimbali wa Elimu na Taasisi binafsi kwa lengo kuunda mkakati wa Taifa wa maendeleo ya stadi za kazi ili kuondoa mwanya uliopo baina ya Elimu ya cheti na ustadi au ujuzi unaotakiwa kwenye soko la ajira.

 

Balozi Sefue amesema lengo kuu ni kutafuta njia ambayo itasaidia kutengeneza mfumo utakaosaidia kujenga mkakati wa kuendeleza ufundi au ujuzi wa mtu uwe na tija kwake kwa kuwa na sera maalum ili kupunguza tatizo la ajira lilopo.

 

Comments are closed.