PANDE zinazozozana nchini Sudan Kusini zinafanya mazungumzo nchini Ethiopia hii leo ikiwa ni siku ya mwisho ya mazungumzo ya amani kabla ya vikwazo vya kimataifa kuwekewa pande zote.
Lakini serikali ya Sudan Kusini pamoja na waasi wamesema huenda wakahitaji muda zaidi kutatua maswala kama vile mgawanyo wa madaraka katika serikali ya mpito.
Mwakilishi maalum wa Muungano wa Ulaya, Alexander Rondo, ameonya kuwa ucheleweshwaji wa kufikia makubaliano hautavumiliwa. Marais wa Uganda, Kenya na Ethiopia pia wanashiriki mazungumzo hayo.