WAENDESHA mashtaka nchini Brazil wamefungua mashtaka ya rushwa na usafishaji wa fedha chafu dhidi ya spika wa congress, Eduardo Cunha.
Cunha anatuhumiwa kupokea dola milioni tano kama rushwa ili kuingia katika mikabata na shirika la mafuta la serikali, Petrobras.
Bwana Cunha amekana tuhuma hizo na kusema zina ushawishi wa kisiasa.