UFARANSA NA UINGEREZA KUIMARISHA USALAMA

UFARANSA NA UINGEREZA KUIMARISHA USALAMA

Like
326
0
Friday, 21 August 2015
Global News

MAAFISA kutoka Ufaransa na Uingereza wamesaini makubaliano ya kuimarisha ushirikiano wa usalama katika kivuko kimoja muhimu cha mpakani, huku wakitangaza hatua zikiwemo teknolojia ya kisasa ili kuwadhibiti wahamiaji na waomba hifadhi wanaojaribu kuingia Uingereza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Bernard Cazeneuve na mwenzake wa Uingereza Theresa May, wamesaini makubaliano  ya muafaka jana katika mji wa bandari wa Calais, ambako mamia ya watu wamejaribu kuvuka mpaka na kuingia Uingereza kutokea Ulaya katika kipindi cha mwaka huu ulioshuhudia ongezeko la shinikizo la wahamiaji.

Comments are closed.