WAZIRI MKUU wa Ugiriki Alexis Tsipras amejiuzulu na kuitisha uchaguzi ufanyike mapema.
Hatua hiyo inaonekana kuwa juhudi za kuzima uasi ndani ya chama chake cha Syriza na kuimarisha uungwaji wake mkono wa mpango wa tatu wa uokozi wa uchumi wa nchi hiyo inayokabiliwa na madeni, ikiwa ni hatua ya kwanza ambayo imeidhinishwa na mawaziri wa fedha wa mataifa ya kanda ya euro wiki hii.