UMOJA wa madereva wa bodaboda wilaya ya IIala (UMABWILA) wamesema kuwa vyama vya bodaboda havifungamani na siasa na kila mwanachama anahaki ya kupenda na kushabikia chama chochote cha siasa.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam leo Makamu mwenyekiti wa Umoja huo, BASHIRU KASHAIJA amesema kuwa watashirikiana na chama ambacho kimesaidia kuwezesha bodaboda kuwa chombo rasmi cha usafirishaji.