MASHEKHE NA WALIMU WA MADRASA WAMETAKIWA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUPENDA AMANI

MASHEKHE NA WALIMU WA MADRASA WAMETAKIWA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUPENDA AMANI

Like
406
0
Thursday, 27 August 2015
Local News

MASHEKHE na Walimu wa Madrasa wametakiwa kuwahamasisha Wananchi kupenda Amani ili waepuke kujiingiza katika makundi yanayoweza kuvunja amani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu.

 

Hayo yameelezwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi alipokuwa akifungua mafunzo ya Haki za Binaadamu yaliyoandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar.

 

Katika mkutano huo Sheikh Omary amesema Masheikh na Walimu hao ndio Wasimamizi wakuu wa Amani katika maeneo mbalimbali ikiwemo Miskitini na hata ndani ya Nyumba zao  hivyo ni muhimu kuliwekea msisitizo wa kutosha suala hilo kwa manufaa ya Taifa.

 ZNZ2

Comments are closed.