IKIWA Zimebaki saa chache kuanza kutumika kwa sheria ya makosa ya mitandao na miamala ya kielektroniki, Watanzania Nchini wametakiwa kuwa makini na Kuzingatia matumizi salama na sahihi ya mitandao ili kujiepusha na adhabu zitakazo tolewa kwa yeyote atakaye kiuka sheria hiyo
Akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es salaam, Waziri wa Mawasiliano ya Sayansi na Technolojia PROFESA MAKAME MBARAWA amesema kuwa Sheria hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza na hatimaye kuondoa kabisa matumizi mabaya ya mitandao na kwamba Serikali ina imani na sheria hii kuwa itakuwa ni hatua moja ya kimaendeleo Nchini