MAELFU ya wahamiaji wanaendelea kuwasili Ugiriki, huku serikali ikijiandaa kwa mazungumzo ya kujadili mbinu za kukabiliana na wahamiaji wengi wanaofika katika fukwe za taifa hilo.
Meli mbili zilizobeba zaidi ya watu 4,200 zilisafiri hadi bandari ya Piraeus, usiku baada ya kuondoka kisiwa cha Lesbos.
Mamia ya watu, wengi kutoka Mashariki ya Kati, bado wamekwama nje ya kituo cha reli nchini Hungary, baada ya polisi kuwazuia kusafiri kuingia EU.