ASILIMIA 60 YA WAFANYAKAZI WAPO HATARINI KUPATA MAGONJWA SUGU

ASILIMIA 60 YA WAFANYAKAZI WAPO HATARINI KUPATA MAGONJWA SUGU

Like
256
0
Thursday, 03 September 2015
Local News

ZAIDI ya Asilimia 60 ya watumishi mbalimbali wako katika hatari ya kupata magonjwa sugu kama shinikizo la damu magonjwa ya moyo na kisukari kutokana na tabia hasi ya jinsi wanavyoendesha maisha yao ya kila siku.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania –TACAIDS Dokta FATUMA MRISHO katika zoezi la upimaji wa afya kwa watumishi wasio pungua laki tatu kutoka sekta za uma na binafsi na kugundua kuwa watumishi wengi hawafuati ushauri wa wataalamu wa afya.

Mwenyekiti huyo amebainisha kuwa zoezi hilo limezunguka mikoa 12 nchini kuanzia Septemba mwaka jana na kumalizika Mei mwaka huu ambapo jumla ya watumishi waliojitokeza kupima afya zao walikuwa wanaume Elfu kumi na miamoja arobaini na tisa sawa na asilimia 57 na wanawake Elfu saba mia tano na tisini na moja sawa na asilimia 43 ambapo waliogundulika na virusi vya ukimwi walikuwa wanawake asilimia 51 na wanaume walikuwa asilimia 49.

Comments are closed.