UTAFITI wa maswala ya gesi uliofanywa na taasisi ya utafiti ya REPOA kwa kushirikiana na kituo cha maendeleo duniani umeonyesha kua Watanzania wanahitaji gesi iweze kuchimbwa ili isaidie kwenye kuboresha maisha na huduma za jamii.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam baada ya kuwasilisha Ripoti ya utafiti huo mtafiti kutoka kituo cha maendeleo duniani Mujobi Moyo amesema Watanzania wengi wametaka gesi iwe ni sababu ya kuboresha huduma za afya, huduma za elimu, kuboresha miundombinu pamoja na kusaidia upatikanaji wa ajira nchini ili kuinua hali zao kimaisha.