SHIRIKA la umeme nchini TANESCO kwa kushirikiana na jeshi la polisi wamewakamata watu watatu wanaohusika na kuiba vifaa muhimu katika TRANSFOMA mbili za wilaya ya Ilala na kupelekea wakazi wa maeneo hayo kukosa huduma ya umeme.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja wa Tanesco, Ilala ATHANASIUS MANGALI, Amesema kuwa kumekuwa na wizi wa vifaa muhimu katika transfoma ambavyo vinapelekea kifaa hicho kushindwa kusambaza umeme ipasavyo.
Amesema Tanesco kwa msaada wa karibu kutoka jeshi la polisi jana majira ya usiku wameweza kuwakamata wahalifu hao na mpaka sasa wanashikiliwa na polisi.