IOC KUFADHILI MICHEZO KWA WAKIMBIZI

IOC KUFADHILI MICHEZO KWA WAKIMBIZI

Like
271
0
Saturday, 05 September 2015
Slider

Shirikisho la michezo ya Olimpiki, IOC, leo limetangaza hazina ya dola millioni mbili, ambazo zitatolewa kwa Kamati ya Kitaifa ya olimpiki ya nchi wanachama kufadhili miradi itakayowasaidia wakimbizi katika mataifa yao.

Rais wa IOC, Thomas Bach, amesema kuwa kama shirikisho la michezo ya olimpiki, imehuzunishwa na habari zainazowahusu wakimbizi, katika siku za hivi karibuni.

Amesema IOC imekuwa ikifuatilia matukio yanayojiri katika eneo la Mashariki ya Kati, Afrika na Ulaya na wao wanataka kutumia michezo kuwaleta wanainchi pamoja, hasa kuwasaidia wakimbizi.

Amesema IOC imekuwa na ushirikiano mwema na Umoja wa Mataifa na shirika lake linalowahudumia wakimbizi UNHCR na watashirikiana kuhakikisha fedha hizi zimewanufaisha wakimbizi na zaidi ya yote kujaribu kuleta amani na utengamano.

Kamati za kitaifa za Olimpiki na mashirika mengine sasa zitahitajika kutuma maombi yao ya ufadhili kwa IOC, kuhusu miradi wanayotaka kufanya.

Bach, amesema kutokana na hali ya mzozo huo kwa sasa, uchunguzi wa miradi hiyo na usambazaji wa fedha utaharakihwa.

Mwaka uliopita, aliyekuwa rais wa IOC, Jack Rogge, alikamilisha ujumbe wake wa kwanza kama mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, anayehusika na masuala ya vijana wakimbizi na michezo.

Comments are closed.